Yamesasishwa 24/10/2026. PDF Haraka ni huduma ya EKJ Dynamics, Tanzania.
1. Huduma
PDF Haraka inatoa zana za kuunganisha, kugawanya, kupunguza ukubwa, kubadilisha, kulinda na kufungua mafaili ya PDF. Zana hizi zinafanya kazi ndani ya kivinjari chako: nyaraka unazochagua zinashughulikiwa kwenye kifaa chako na hazitumwi kwenye seva zetu, isipokuwa ukichagua “Hifadhi kwenye mafaili yangu”.
2. Akaunti
- Unaweza kutumia zana bila akaunti, kwa mafaili hadi ukubwa unaoonyeshwa kwenye ukurasa.
- Ili kufungua akaunti unatoa namba yako ya simu na jina kamili, kisha unathibitisha namba kwa msimbo wa SMS wa mara moja. Hakuna nenosiri. Una wajibu wa kulinda upatikanaji wa namba yako ya simu.
- Lazima utumie jina lako halisi na namba ya simu iliyo yako.
3. Vifurushi vya wiki na malipo
- Vifurushi vya kulipia vinaruhusu mafaili makubwa zaidi kwa idadi ya wiki uliyolipia. Bei zinaonyeshwa kwa shilingi za Kitanzania (TZS) kwa wiki kabla ya kulipa.
- Unalipa kwenye Lipa Namba inayoonyeshwa kwenye tovuti na kuandika namba ya muamala. Kifurushi chako kinaanza tukishahakiki malipo, kwa kawaida ndani ya saa chache katika siku za kazi.
- Vifurushi havijirudii vyenyewe. Wiki ulizolipia zikiisha, akaunti inarudi kuwa ya Bure; mafaili uliyohifadhi yanabaki hadi tarehe yake ya kufutwa.
- Malipo yasipolingana na namba ya muamala uliyoandika, kifurushi hakitaanzishwa na tutawasiliana nawe. Malipo ya wiki zilizokwisha anza hayarudishwi, isipokuwa pale sheria za Tanzania zinapotaka. Michango ni ya hiari na hairudishwi.
4. Mafaili yako
- Tumia mafaili unayoyamiliki au unayoruhusiwa kuyatumia tu. Usitumie huduma hii kwa jambo lolote lisilo halali, kwa mafaili yanayokiuka haki za wengine, au kujaribu kuidhuru huduma.
- Mafaili yaliyohifadhiwa yamesimbwa (encrypted) kwenye seva yetu, yanaonekana kwa akaunti yako tu, na yanafutwa yenyewe baada ya muda unaoonyeshwa kwenye ukurasa (au muda mrefu zaidi ukichagua kuyaweka). Mafaili yaliyofutwa hayawezi kurudishwa. Weka nakala yako ya kila kitu muhimu.
- Nenosiri unaloweka kwa “Linda PDF” halitumwi kwetu na haliwezi kurejeshwa. Ukilisahau, faili haliwezi kufunguliwa.
- Kupunguza ukubwa, kubadilisha na kusoma maandishi ya picha (OCR) hufanyika kiotomatiki na huenda visiwe kamili. Hakiki matokeo kila mara kabla ya kuyategemea.
5. Faragha
- Tunahifadhi namba yako ya simu, jina, kifurushi, malipo na mafaili uliyohifadhi. Tunatumia namba yako kukuingiza tu na kuhusu akaunti au malipo yako; hatuiuzi wala kuishiriki, isipokuwa kwa mtoa huduma wa SMS anayetuma misimbo yako ya kuingia au pale sheria inapotaka.
- Tunahesabu wageni na matumizi ya zana ili kuboresha huduma. Takwimu hizi hazihifadhi anwani yako ya IP wala maudhui ya mafaili.
- Unaweza kutuomba tufute akaunti yako na mafaili uliyohifadhi wakati wowote.
6. Upatikanaji na dhima
Tunajitahidi kuhakikisha PDF Haraka inapatikana na iko salama, lakini huduma inatolewa “kama ilivyo”, bila uhakika kwamba itapatikana kila wakati au bila hitilafu. Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, EKJ Dynamics haiwajibiki kwa upotevu wa data, mapato au hasara nyingine zisizo za moja kwa moja zitokanazo na matumizi ya huduma. Dhima yetu yote ina kikomo cha kiasi ulicholipa katika wiki nne zilizopita.
7. Mabadiliko na sheria
Tunaweza kusasisha masharti haya; tarehe iliyo juu inaonyesha toleo la karibuni, na kuendelea kutumia huduma kunamaanisha unayakubali. Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.